Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kukata msaada wa kifedha kwa serikali ya Palestina, kwa madai kuwa Marekani inawalipa mamilioni ya dola kwa mwaka, huku hakuna chochote inachoambulia, hakuna cha shukrani ama heshima kutoka kwa taifa hilo.

Amesema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo kwakuwa Wapalestina hawana mpango wowote wa kuwa na mazungumzo ya maridhiano ya amani na Israel na kuhoji uhalali wa Marekani kuendelea kujitoa kwa kiasi hicho.

Aidha, Mwezi uliopita rais wa Palestina, Mahmoud Abbas alitoa tamko la taifa lake kutokuwa tayari kupokea mpango wowote wa amani kutoka Marekani, baada ya Marekani kutangaza kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.

Hata hivyo, rais wa Marekani, Donald Trump ameendelea na msimamo wake wa kuutambua mji wa Jerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel.

 

Video: Babu Seya, Papii Kocha waula tena, Clouds washtukia jambo sakata la Masoud Kipanya
Ombi la Ray C kwa JPM, 2018