Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa onyo kali kwa mtu yeyote anayeshirikiana kibiashara na Iran kufuatia hatua yake ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo.
Vikwazo hivyo vilianza kutekelezwa mara moja huku vingine vikali vinavyohusiana na mafuta vinatarajiwa kuanza mwezi Novemba.
“Yeyote atakayefanya biashara na Iran hataruhusiwa kufanya biashara na Marekani,”rais Trump alituma ujumbe wa twitter.
Aidha, kwa upande wake Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema kuwa hatua hizo ni vita vya kiakili ambavyo vinalenga kuleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Iran.
Hata hivyo, vikwazo hivyo vinafuatia hatua ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya kinyuklia ya Iran mapema mwaka huu, yalioafikiwa wakati wa utawala wa rais Barrack Obama ambayo yaliilazimu Iran kusitisha mpango wake wa kinyuklia huku vikwazo dhidi yake vikiondolewa.
-
Umoja wa Mataifa wainyoshea kidole Korea Kaskazini
-
Luiz Lula Da Silva kugombea tena Urais Brazili
- Trump kumpokea Kenyatta ‘White House’, aweka historia