Rais wa Marekani, Donald Trump amesema nchi yake inafanya tathimini ya kambi zake mbili za kijeshi zilizopo Iraq katika mji wa Irbil na Al Asad baada ya kushambuliwa kwa makombora kadhaa na Iran.

Kiongozi huyo amesema anatarajia kutoa tamko muda sio mrefu kufuatia shambulio hilo la kigaidi dhidi ya kambi zake za kijeshi.

Taarifa hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika.

“Kila kitu kipo sawa, kambi zetu mbili za jeshi la Marekani zilizopo Iraq zimeshambuliwa na Iran tunafanya tathimini kujua kama kuna waliopata madhara au uharibifu wowote wa mali, yote kwa yote tuna vifaa bora vya kivita kuliko nchi yeyote duniani, nitatoa tamko hivi punde” amesema Trump.

Aidha imetangazwa kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu Qasem Soleimani aliyeuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani mjini Baghdad, kufuatia agizo la rais wa Marekani Donald Trump.

Ambapo mashambulio hayo ya kambi za jeshi la Marekani yalifanyika saa kadha baada ya mazishi ya Kamanda Mkuu, Soleimani ambaye inasadikika kuwa Trump alihusika na kifo chake akidai kuwa ni gaidi mkubwa aliyehusika na vifo vya mamia ya wanajeshi wa Marekani.

Hata hivyo Uingereza imechukua hatua ya tahadhari kwa kuweka tayari manuari yake ya kivita na helikopta za kijeshi baada ya kuongezeka kwa hali ya taharuki mashariki ya kati, amesema waziri wa ulinzi Ben Wallace.

 

Video: Vita mpya Chadema, Marekani, Iran zaiweka dunia njia panda
Makumi wafariki wakipokea mwili wa Kamanda wa Iran aliyeuawa na Marekani