Rais wa Marekani, Donald Trump ameagiza vikosi kadhaa vya jeshi la nchi hiyo kuingia nchini Somalia kwa lengo la kutoa mafunzo kwa vikosi vinavyopambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab na kushiriki mapambano hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kupeleka vikosi vya jeshi lake tangu ilipolazimika kuviondoa nchini humo mwaka 1994, ingawa washauri wake wa masuala ya kigaidi waliendelea kuwa nchini humo.

Mwezi uliopita, Rais Trump aliidhinisha maagizo ya kuchukua hatua kali za kijeshi dhidi ya kundi la Al-Shabaab.

Mwaka 1993, wanajeshi 18 wa kikosi maalum cha jeshi la Marekani waliuawa nchini Somalia, tukio ambalo liliigizwa kwenye filamu ya Hollywood inayoitwa ‘Black Hawk Down’.

Tukio la kuuawa kwa wanajeshi hao wa Marekani na kudunguliwa kwa ndege mbili za kivita za Marekani jijini Mogadishu kiliishtua nchi hiyo na kupelekea kuviondoa vikosi vyake muda mfupi baadae.

Wananchi wakiangalia mabaki ya ndege za Marekani zilizodunguliwa Somalia, mwaka 1993

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 16, 2017
Video: "Tumejiandaa kwa vita kamili'' - Korea Kaskazini

Comments

comments