Rais wa Marekani, Donald Trump ameunga mkono hatua iliyofikiwa na Bunge la nchi hiyo ya kuiwekea vikwazo nchi ya Urusi mara baada ya kubainika kuwa ilidukua uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais Trump, ameunga mkono makubaliano hayo yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi kwa kuwa Marekani imesema kuwa huo ulikuwa ni uchokozi
Aidha, Bunge la Congress linataka Urusi iadhibiwe kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani,kwani hatua ya kuiwekea vikwazo Urusi itakuwa ni fundisho na onyo kwa nchi hiyo.
Hata hivyo, kupitishwa kwa sheria hiyo na bunge la Congress kutamnyima uwezo Rais Trump kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa na bunge dhidi ya Urusi kwakuwa kina lengo la kumpunguzia madaraka.