Rais wa Marekani, Donald Trump amevitaka vyombo vya habari kuacha chuki isiyokuwa na kikomo baada ya kutoa taarifa ya vilipuzi vilivyokuwa vimetumwa kwa watu mashuhuri nchini Marekani.

Ameyasema hayo mara baada ya vifurushi hivyo kutumwa kwenye chombo cha habari cha CNN na kwa viongozi wa juu wa chama cha Democrats ikiwajumuisha Barack Obama na Hillary Clinton.

Aidha, mpaka sasa hakuna kifurushi chochote kilicholipuka, huku shirika la ujasusi la nchi hiyo FBI bado linawatafuta wale wote waliotuma mizigo hiyo.

Rais Trump amedai kuwa atahakikisha watu waliotuma vifurushi hivyo wanakamatwa huku akivitaka vyombo vya habari kuacha kutoa taarifa ambazo hazina ukweli wowote.

Hata hivyo rais Trump hakuweka wazi ni jambo gani ambalo amelenga kuwafanyia watu waliohusika na kupeleka vifurushi hivyo.

 

Al Masry wasusa DR Congo, waipeleka AS Vita Club fainali
Rais George Weah atangaza elimu bure vyuo vikuu