Mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump ametembelea kanisa moja la watu weusi mjini Detroit katika kuhamasisha kuungwa mkono kwa watu walio wachache kutoka kwa mpinzani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton.

Ameuambia umati wa watu kwamba anaelewa kwamba Wamarekani weusi wanakabiliwa na ubaguzi.Kura za maoni zinaonyesha kuwa Trump  yuko nyuma ya bi Clinton kwa umaarufu ana ufuasi mdogo miongoni mwa Wamarekani weusi na wapiga kura wa Hispanic.

Bwana Trump aliwasili katika kanisa hilo huku kukiwa na maandamano dhidi yake yaliofanyika nje ya kanisa hilo.

Akiwa ndani ya kanisa hilo alifanya mahojiano ya moja kwa moja na askofu Wayne T Jackson.

 

Ajali Yasababisha Vifo Vya Watu 35 Afghanistan
Ratiba Ya Leo Michezo Kufuzu AFCON 2017