Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ameachiliwa kwa dhamana katika jela ya kaunti ya Fulton ya mji wa Atlanta uliopo jimbo la Georgia, baada ya kujisalimisha kufuatia kufunguliwa mashtaka kwa kujaribu kubadili matokeo ya uchaguzi wa 2020, na uhalifu mwingine.

Trump, alishtakiwa mapema mwezi Agosti, 2023 kwa kukiuka sheria za jimbo la Georgia za ubadhirifu na kutenda uhalifu mwingine, akikabiliwa na mashtaka 13 na hapo jana (Agosti 24,2023), alichukuliwa alama za vidole na picha yake akiwa jela.

Hakuna rais mwingine wa zamani wa Marekani ambaye ameshtakiwa kwa makosa ya jinai, lakini Trump sasa anakabiliwa na kesi nne, na jumla ya mashtaka 91 kwa madai ya vitendo vyake vya kabla, wakati na baada ya muhula wake mmoja wa urais uliomalizika mwaka 2021.

Washtakiwa wengine, akiwemo wakili wake wa zamani Rudy Giuliani, walijisalimisha kwenye jela siku chache zilizopita na mapema wiki hii, Trump alikubali dhamana ya dola 200,000 na masharti mengine ya kuachiliwa, ikiwa ni pamoja na kutotumia mitandao ya kijamii kuwatisha washtakiwa wenzake au mashahidi katika kesi hiyo.

Rais Samia azungumza na Rais wa Brazil
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 25, 2023