Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Marekani itajitoa katika mkataba wa enzi za vita baridi ambao unafuta aina ya silaha za nyuklia kutokana na ukiukaji unaofanywa na Urusi.

Mkataba huo unaojulikana kama Intermediate-Range Nuclear Forces Treaty, uliojadiliwa na  kufikia makubaliano wakati wa utawala wa rais Ronald Reagan na kiongozi wa Urusi wakati wa enzi za Umoja wa Kisovieti, Mikhail Gorbachev mwaka 1987, unataka kuondolewa kabisa kwa makombora ya kinyuklia ya masafa mafupi na kati  pamoja na makombora ya bara hadi bara kwa nchi  zote.

“Urusi kwa bahati mbaya haijatimiza makubaliano hayo kwa hiyo tutasitisha makubaliano hayo na tutajitoa,” amesema Trump  alipokuwa akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wa hadhara mjini Nevada.

Trump amesema kuwa Marekani itatengeneza silaha hadi pale Urusi na China zitakapokubali kusitisha utengenezaji wa silaha.

Aidha, China haimo katika mkataba huo na imewekeza kwa kiasi kikubwa katika makobora ya masafa marefu kama sehemu ya mkakati wa kuzuia kuingiliwa katika maeneo yake, wakati mkataba wa INF umepiga marufuku Marekani  kuwa na makombora ya masafa marefu yanayorushwa kutokea ardhini ama makombora yenye uwezo wa kurushwa  kwa umbali wa kilometa 500 na 5,500.

Hata hivyo, Naibu waziri wa mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Ryabkov katika matamshi yaliyoripotiwa na shirika la  habari la Urusi TASS, amesema hatua ya Marekani kuchukua uamuzi wa kujitoa bila makubaliano na upande wa pili itakuwa hatua ya hatari sana.

 

Prof. Ndalichako aagiza waliofutiwa usajili UDSM warejeshwe
Video: Treni yaua 18 yajeruhi 170 China