Wagombea urais wa Marekani Donald Trump wa chama cha Republican na Joe Biden mgombea kutoka chama cha Democratic wanatarajia kufanya mdahalo wa mwisho siku ya Ijumaa na watayarishaji wameweka masharti maalum kuzuia hali ya wagombea hao kulumbana bila mpangilio kama ilivyotokea mara ya kwanza.
Taarifa hiyo iliyotolewa na watayarishaji wa mdahalo huo imeeleza kuwa kutakuwa na kitufe cha kufunga kipaza sauti cha kila mgombea ili kuzuia hali ya kuingiliana wakati wa kuzungumza ili kuzuia hali iliyojitokeza katika mdahalo wa kwanza.
Meneja wa kampeni ya Trump, Bill Stepien amesema kwamba rais huyo yuko tayari kufanya mdahalo huo na Joe Biden bila kujali mabadiliko ya dakika za mwisho ya sheria.
Zaidi ya Wamarekani milioni 30 wamekwisha piga kura zao, wakipunguza uwezekano wa Trump kubadilisha hali ya mwelekeo katika nchi hiyo ambayo inaonesha kuwa yuko nyuma katika maoni ya wapiga kura kitaifa na katika majimbo.