Rais wa Marekani, Donald Trump ameapa kuiangamiza Korea Kaskazini endapo itaendelea na mpango wake wa kufanya majaribio ya silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu.

Ameyasema hayo mara baada ya Ikulu ya nchi hiyo kutoa ratiba ya ziara ya Rais huyo katika mataifa matano barani Asia mwezi Novemba ili kushiriki katika mikutano ya ukanda huo ya kujadili mambo mbalimbali.

Aidha, Ikulu ya Marekani imezitaja nchi ambazo Rais Trump atazitembelea ndani ya siku kumi na moja za ziara yake barani humo kuwa ni pamoja na washirika wake wakubwa  ambao ni Japan, China, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino na Hawaii.

Ziara hiyo ya Rais, Trump inatarajiwa kuimarisha harakati zake za kimataifa za kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini ambayo amekuwa akiipinga kuhusiana na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Hata hivyo, Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana maneno ambayo yamesababisha mvutano mkali kati kuhusiana na majaribio mbalimbali ya silaha za nyuklia yanayofanywa na Korea Kaskazini katika miezi ya hivi karibuni

Hemed Phd aeleza familia ‘ilivyomvuta shati’...
Kenya yaandaa muswada kwa ‘dharura’ kubadili sheria ya uchaguzi