Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa ataagiza nyaraka za siri za upelelezi wa mauaji ya Rais wa 35 wa nchi hiyo, John Kennedy kuwekwa hadharani.

John Kennedy ambaye alifahamika zaidi kwa jina la JFK, aliuawa kwa kupigwa risasi na ‘watu wasiojulikana’ Novemba 22 mwaka 1963, ikiwa ni miaka mitatu tu tangu awe rais wa nchi hiyo.

Baadhi ya watu wamekuwa wakituhumiwa kuhusika kupanga tukio hilo lakini ripoti kamili ya upelelezi imekuwa ni siri kubwa.

Rais Trump amewahi kuwataja watu kadhaa wakati wa kampeni zake za kuwania nafasi ya urais mwaka 2016 akiwahusisha kupanga njama ya mauaji hayo.

Trump alimtuhumu hadharani hasimu wake, Seneta Ted Cruz kuwa alishiriki njama za kumuua John Kennedy, lakini hajawahi kuomba radhi kwa kutoa tuhuma hizo nzito.

“Kwa kuzingatia upokeaji wa taarifa za ziada, kama Rais, nitaruhusu kuwekwa wazi kwa nyaraka za siri za mauaji ya JFK ambazo zilizuiwa kwa muda mrefu,” Rais Trump ametweet.

Hata hivyo, amesema kuwa anametoa nafasi kwa baadhi ya nyaraka za siri kuendelea kutunzwa bila kuwekwa hadharani.

Afisa kutoka Ikulu ya Marekani aliwaambia waandishi wa habari kuwa nyaraka hizo zinapaswa kuwekwa wazi ili kutekeleza sera ya uwazi, isipokuwa pale ambapo vyombo husika vya usalama vitakapotoa sababu za msingi za kuendelea kuzifanya baadhi ya nyaraka kuwa siri.

M.I wa Nigeria amshtaki Nas kwa utapeli
Video: Mkakati wa kumng'oa Spika Ndugai wapikwa, Kitaeleweka