Rais wa Marekani, Donald Trump amepanga oparesheni ya kuanza kuwafukuza wahamiaji wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini humo, licha ya kupingwa na chama cha Democratics.
Oparesheni hiyo inasemekana kwamba inaweza kuanza kutekelezwa mwishoni mwa juma hili, baada ya kuahirishwa na Trump mwishoni mwa mwezi uliopita.
Aidha, oparesheni hiyo ina lengo la kuwafukuza watu ambao wameamriwa kurejea katika nchi zao, zikiwemo familia za wahamiaji ambazo kesi zao zilikuwa zikifuatiliwa kwa haraka na majaji katika jumla ya miji 10 kama vile Chigaco, Los Angeles, New York na Miami.
Hatua hizo zimeibua hasira na wasiwasi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wahamiaji na wabunge.
Hata hivyo, Trump alitangaza kwenye ukuara wake wa kijamii mwezi uliopita kwamba oparesheni hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuwafukuza mamilioni ya watu wanaoishi Marekani kinyume cha sheria.