Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kuhutubia kongamano la uchumi duniani linalotarajiwa kufunguliwa hii leo na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, mjini Davos nchini Uswisi.

Ajenda kubwa ya mwaka huu ya kongamano hilo la WEF ni kutafuta mustakabali wa pamoja katika dunia iliyofarakana, ambapo inapingana moja kwa moja na sera ya rais wa Marekani Donald Trump ya “Marekani kwanza”

Aidha, Rais wa kongamano hilo, Borge Brende amesema kuwa kongamano hilo la wakuu 70 wa serikali mbalimbali duniani pamoja na wafanyabiashara wenye nguvu linaweza kuleta mchango mkubwa kuelekea kukabiliana na vikwazo vya sasa katika sekta ya biashara duniani.

Naye Waziri mkuu wa Canada, Justin Tradeau anatarajiwa kuwasilisha ajenda kuu ya mwaka huu ya mataifa yenye uchumi imara G7. ambapo Canada inachukua uenyekiti wa kundi hilo mwaka huu.

Hata hivyo, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewataka wafanyabiashara na wanasiasa katika kongamano hilo kuandaa mazingira yatakayoruhusu ujenzi wa jamii inayohusisha makundi yote.

 

Ridhiwani: Hayo si maneno yangu
Nabii Tito ashikiliwa na Polisi