Rais wa Marekani, Donald Trump amepanga kuiondoa Marekani katika mkataba wa nyuklia kati ya nchi za Magharibi na Iran ili kuiadhibu nchi hiyo kutokana na hatua za hivi karibuni za kuanza kufanya majaribio ya silaha za nyuklia.

Trump aliukosoa mkataba huo tangu enzi za kampeni zake za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo huku akimtuhumu, mtangulizi wake Rais  Mstaafu Barrack Obama kuwa alifanya makosa kwani kuna mapungufu makubwa.

Aidha, mkataba huo ulisainiwa mwaka 2015 kwaajili ya kuidhibiti Iran na mpango wake wa utengenezaji na uboreshaji wa silaha za nyuklia ambao umekuwa ukipingwa mara kwa mara na Marekani.

Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uchina, Urusi na Uingereza ambao ni wahusika wakubwa katika mkataba huo ambao uliondoa baadhi ya vikwazo ambavyo viliwekwa dhidi ya Iran kuhusu masuala ya biashara ya kimataifa na kuuza mafuta, vinauunga mkono mkataba huo.

Hata hivyo, katika hotuba yake ya kwanza aliyoitoa kaika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,Trump alisema mkataba huo uliosainiwa na mtangulzii wake Barack Obama kuwa ni wa aibu na haufai.

Selasini na wapiga kura wake kuamua kuhusu Ben Saanane
Marekani yaiondolea vikwazo Sudan