Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa hajui chochote kuhusu malipo ya fedha za Kimarekani dola 130,000 yaliyolipwa na wakili wake kwa mchezaji filamu za utupu, Stormy Daniel kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.
Ameyasema hayo mara baada ya kuulizwa ni kwanini wakili wake alimlipa fedha hizo muigizaji wa picha za utupu nchini humo.
Aidha, katika majibu yake, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa ni bora akaulizwa wakili, Michael Cohen kwanini alifanya malipo hayo na si yeye.
Muigizaji huyo amesema kuwa alifanya tendo la ndoa na Rais Trump mwaka 2006 lakini Trump amekanusha vikali madai hayo akisema ni uzushi mtupu.
Hata hivyo, Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, amesema kuwa alisaini makubaliano ya kutokutoa siri kuhusu mashusiano yake na Rais Trump na kulipwa dola za Marekani 130,000 mwezi Oktoba 2016, kabla ya uchaguzi wa urais.