Uongozi wa Simba SC, umeibuka na kusema kuwa, hakuna kitakachowazuia wao kubeba makombe katika msimu wa 2023/24 kutokana na usajili kufanyika kitaalam.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wao Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii watakaocheza leo Alhamisi (Agosti 10) dhidi ya Singida Fountain Gate kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba SC ni Willy Onana, Fabrice Ngoma, Luis Miquissone, Che Malone Fondoh Aubin Kramo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah “Try Again’ amesema usajili umefanyika kutokana na malengo ya timu kwa msimu wa 2023/24.

Try Again amesema, mara baada ya usajili huo kufanyika, mashabiki wasubirie kuona ubora wa kila mchezaji bila ya kocha kuingiliwa katika upangaji wa kikosi.

Ameongeza kuwa, siku zote kocha anaangalia mchezaji mwenye utayari atakayeipa matokeo mazuri timu, na sio kitu kingine, kwani yeye ndiye anaamua yupi acheze.

“Usajili wetu wa msinu huu umefanyika kitaalamu kutokana na malengo na mipango ya timu iliyokuwepo hivi sasa ili kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu.

“Kusajili ni kitu cha kwanza na ndani ya uwanja ni kitu cha pili, mwisho wa siku kocha ndiye anayeamua mchezaji gani wa kuanza katika kikosi cha kwanza,

“Lakini kitu kingine ni utayari wa mchezaji mwenyewe mazoezini, pia kuna majeruhi na vitu vingine vingi kwa wachezaji, hivyo Wanasimba waondoe hofu,” amesema Try Again.

Polisi kuendeleza ushirikishaji jamii kutokomeza uhalifu
Mkataba uwekezaji wa Bandari ni halali - Mahakama