Beki wa kushoto na Nahodha Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesemna ujio wa Kocha Abdelhak Benchikha umerudisha ari ya upambanaji kwa wachezaji wa timu hiyo na anaamini wanakwenda kufanya vizuri kwenye michezo itakayowakabili katika mashindano yote wanayoshiriki msimu huu 2023/24.

Simba SC mwanzoni mwa juma hili ilimtambulisha Kocha wa zamani wa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika USM Alger ya Algeria, Benchikha kuwa kocha mpya wa timu hiyo na kabla ya kuanza kazi ya kuanza kukinoa kikosi hicho alizungumza na wachezaji wa timu hiyo kuwapa mikakati na majukumu anayotaka wayatimize kufikia malengo.

Tshabalala amesema kikao na kocha huyo kimeifanya timu hiyo ilizaliwe upya na kila mchezaji ana shauku ya kutekeleza yale waliyokubaliana na mkufunzi huyo aliyeiongoza USM Alger kushinda Kombe la Shirikisho la Soka Barani Afrika msimu uliopita 2022/23.

“Unajua maneno yalikuwa mengi mtaani baada ya kufungwa na Young Africans, ndio maana unaona mechi zilizofuata dhidi ya Namungo FC na Asec Mimosas hatukufanya vizuri.

“Kocha Benchikha ametupa moyo na kurudisha ari ya kila mchezaji na ninaamini kiwango chetu katika mechi zijazo kitakuwa cha juu saa,” amesema Tshabalala.

Amesema mbali na kauli ya ushawishi ya Kocha Benchikha, lakini kingine kilichorudisha faraja kwa wachezaji ni kauli yake ya kutoangalia jina la mchezaji katika upangaji wa kikosi chake ambapo baadhi ya wachezaji hasa wale ambao enzi za Robertinho walikuwa hawapati nafasi ya kuanza mara kwa mara wameifurahia.

PICHA: Simba yawasili salama Francistown-Botswana
Dulla Mbabe kwenda Magereza Dar es salaam