Simba SC imetangaza orodha ya Wachezaji Watatu walioingia Fainali ya kinyang’anyiro cha kuwania Mchezaji Bora wa Nashabiki wa Mwezi Februari wa Klabu hiyo (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Wachezaji waliotajwa kwenye taarifa iliyochapishwa katika vyanzo vya habari vya Klabu hiyo ya Msimbazi ni Beki wa Kati kutoka DR Congo, Henock Inonga, Beki wa Kulia kutoka Tanzania, Shomari Kapombe na Kiungo Mkabaji Kutoka Tanzania, Mzamiru Yassin.

Orodha hiyo imetajwa baada ya kufanywa kwa Mchujo wa wachezaji wengine wawili ambao ni Beki wa Kushoto wa Tanzania, Mohamed Hussein na Kiungo Mkabaji kutoka Mali, Sadio Kanoute ambao waliingia Tano Bora.

Orodha ya Wachezaji Watano iliyotajwa kabla ya kufanywa kwa Mchujo, ilitokana na uwezo uliooneshwa na Wachezaji hao katika Michezo mitano ya mwezi Februari, Mitatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wataanza kupiga Kura kupitia Tovuti ya klabu hiyo, kuanzia Machi Mosi saa Sita Mchana, ili kumpata mshindi wa Mwezi Februari.

Mshindi atakayetangazwa atazawadiwa Tuzo na Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Simba SC Kampuni Emirate Aluminium Profile.

Maafisa watatu TFF wateuliwa CAF
Sababu za Baleke, Bocco , Sakho kuwekwa benchi