Mmoja wa wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Felix Tshisekedi na mwenzake Vital Kamerhe wamerudi Kinshasa kutoka nchini Marekani wakielezea matumaini ya kupata ushindi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu.
Tshisekedi na mwezie waliwasili siku ya jumanne na kusema kuwa kulingana na tafiti iliyofanywa na taasisi moja ya Marekani ambayo hakuitaja yeye na mwenzake Kamerhe wataweza kupata ushindi karibu asilimia 50 za kura wakati wa uchaguzi wa Disemba 23 mwaka huu.
Aidha, kiongozi huyo amesema kuwa uchaguzi huo ni lazima ufanyike kwa kutumia au kutotumia kompyuta ambazo hazitazusha malalamiko nchini humo kwa madai kwamba serikali inaweza kuzitumia mashine kuiba kura.
Hata hivyo, katika uchaguzi huo kuna wagombea 21 wanaoshiriki katika uchaguzi huo wa rais ambapo Tshisekedi na Martin Fayulu ni wagombea wakuu wa upinzani dhidi ya mgombea wa muungano wa vyama vya utawala Emmanuel Ramazani Shadary.
-
Mwanaharakati wa Mazingira kutoka Tanzania kupata tuzo Ujerumani
-
Papa Francis ateua mrithi wa muda wa Askofu Chengula
-
Marekani yatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wahamiaji