Kocha Mkuu wa Kitayosce, Mserbia Goran Kopunovic amesema ameridhishwa na maendeleo ya kiungo kutoka DR Congo Papy Kabamba Tshishimbi baada ya kufanya vyema mazoezini licha ya kuwa nje muda mrefu.

Kiungo huyo wa zamani wa Mbabane Swallows ya Eswatini na Young Africans, aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Ihefu alifanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumizwa na beki wa Simba SC, Joash Onyango wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Novemba 12, mwaka jana.

Kocha Goran amesema nyota huyo kwa sasa yuko fiti kwa asilimia l00 na licha ya kukaa nje muda mrefu bila ya kucheza michezo ya kiushindani ila amefurahishwa na shauku aliyo nayo.

“Ni wachezaji wachache wanaopata majeraha na kurudi kwenye utimamu wa kimwili kwa sababu wengi wanawaza huenda wakaumizwa tena, japo kwa Tshishimbi ni tofauti na imetupa imani kubwa,” amesema.

Akizungumzia maendeleo yake, Tshishimbi amesema urejeo wake ndani ya timu hiyo ni deni kubwa aliloliacha wakati kikosi hicho kikiwa Championship, hivyo karejea kwa ajili ya kulipa fadhila alizopewa.

“Msimu wa mwaka juzi wakati tunashindwa kupanda Ligi Kuu Bara niliumia sana ila nawashukuru viongozi wangu baada ya Ihefu kuleta ofa yao walinikubalia kuondoka, sasa nimerudi tena na wamenipokea kwa heri,” amesema.

David Silva aitabiria makubwa Arsenal
Spika Tulia asaidia Matofali ujenzi jengo la upasuaji