Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL), limeendelea na kampeni yake ya ‘Switch – on’, Mawasiliano kwa wote katika Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na kuelekea Arusha na Manyara.
Kampeni hii ambayo ilizinduliwa tarehe 16 Februari mwaka huu katika kambi ya Jeshi 121 KJ huko Kidagulo, Sangasanga Mkoani Morogoro safari hii imeendelea katika mikoa ya Kaskazini na kuanzia katika kata ya Misalai, Muheza jijini Tanga.
Akizungumza katika kampeni hiyo, Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, AtashastaNditiye amesema mnara huo utasaidia kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na lengo kuu la upatikanaji wa mawasiliano kwa wote.
“Tunaamini kabisa Mnara huu ambao leo tunaenda kuuzindua utasaidia kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na lengo kuu la upatikanaji wa mawasiliano kwa wote” Amesema Nditiye
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba akizungumza na wananchi amesema kuwa Shirika limekuwa likishirikiana pia na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika kuhakikisha huduma ya Mawasiliano inapatikana kwa watanzania wote.
Kampeni hiyo kwa Kanda ya Kazkazini imeendelea katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na itafikia tamati kwa mkoa wa Manyara.