Meneja wa mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain *PSG*, Thomas Tuchel amejivunia kikosi chake baada ya kumaliza michuano ya ndani ya Ufaransa kwa kuwafunga Olympic Lyon, kwenye mchezo wa fainali ya Coupe de la Ligue.

PSG wametwaa taji hilo, kufuatia ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati, ambapo wababe hao wa jijini Paris walipata mikwaju sita huku wapinzani wao Olympic Lyon wakifunga mikwaju mitano.

Hatua ya mchezo huo wa fainali kuamuliwa kwa matokeo ya mikwaju ya penati ilikuja baada ya miamba hiyo kushindwa kutambiana ndani ya dakia 90 kwa kutoka suluhu jana Ijumaa.

Pablo Sarabia aliweka kambani penati ya mwisho iliyowapa ushindi PSG katika fainali hiyo ya Coupe de la Ligue.

Tuchel amesema: “Ni wachezaji wakuaminika wakiwa wanacheza nafurahia kufanya nao kazi hata wakati wa shida tunakuwa pamoja,” alisema kocha wa PSG. Inanifanya niwe na furaha, najivunia na ninafuraha.”

“Hatukupoteza lengo, njaa ya kushinda, kujiamini tukafanikiwa kushinda kwenye mikwaju ya penati hilo tunahesabia pia,” alisema

“Tumeshinda mataji manne, ni jambo zuri na kubwa katika timu yetu na ninafuraha kwa sababu kila mtu anaona ni sawa lakini kiukweli si kazi rahisi kufikia mafanikio haya.

PSG watawakabili Atalanta katika michuano ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya robo fainali jijini Lisbon mwezi Agosti 12.

Spurs, Arsenal zabanana kwa Coutinho
Arteta atamani mafanikio ya Chelsea