Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania, (TUCTA), limesema kuwa serikali inapaswa kuwafikiria na kuwaacha kuendelea na utumishi, watumishi wenye elimu ya darasa la saba.

Limesema kuwa watumishi hao wana uzoefu na ujuzi wa muda mrefu kazini, hivyo kuwaondoa kwa ghafla kutasababisha kuzorota kwa kazi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahaya Msigwa wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio kilichopo jijini Dar es salaam.

“Walioishia darasa bado wana uzoefu na utalaamu mkubwa wa miaka mingi, mfano pale Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) wanajua kila ‘Spea’ katika karakana, kwa hiyo serikali ifanye tathmini ya watumishi hao,”amesema Msigwa

Aidha, amesema kuwa suala la kujiendeleza kwa wafanyakazi hao ni gumu kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kifamilia, hivyo kushindwa kumudu majukumu yote kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, Msigwa ameainisha mikakati ya shirikisho hilo huku akisema litajikita katika kuwaunganisha wafanyakazi ili wawe kitu kimoja.

 

Jaji Mutungi avifunda vyama vya siasa
Video: Kingunge, Maalim Seif wamjadili Lowassa, Mafuriko ya Kibaigwa yatia hofu wabunge