Mwanamuziki maarufu wa R&B nchini Marekani, Robert Sylvester Kelly maarufu R. Kelly amekabiliwa na shutuma mpya kumtumia kimapenzi mvulana mwenye umri wa miaka 17.
Waendesha mashtaka wanadai mwimbaji huyo alimnyanyasa kijana huyo baada ya kukutana naye huko Chicago katika mkahawa wa McDonald’s mnamo 2006.
Wanataka ushahidi wa dhulma hizo na uhalifu mwingine unaodaiwa kutekelezwa naye ambao hakushtakiwa ujumuishwe katika kesi ya Kelly mnamo Agosti.
Kelly anakanusha kumnyanyasa mtu yeyote, na mawakili wake hawajajibu madai haya ya hivi karibuni.
Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy, ambaye jina lake halisi ni Robert Kelly, anatarajiwa kushtakiwa New York mwezi ujao kwa mashtaka yakiwemo unyanyasaji wa kingono wa watoto,kuchukua picha mbaya za watoto, udanganyifu na uzuiaji wa haki.