Klabu ya RS Berkane ya Morocco leo Jumamosi (Agosti 28) imetangaza na kumtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji kutoka DR Congo Tuisila Kisinda.

Berkane ilimsajili Kisinda mwanzoni mwa mwezi huu akitokea Young Africans ya Tanzania kwa ada ya usajili inayoendelea kufanywa siri, kufuatia makubaliano ya pande hizo mbili.

Kwa muda wa majuma matatu sasa, licha ya Kisinda kuonekana akishiriki mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki huko Morocco, alikua hajatanbulishwa rasmi kupitia vyanzo vya habari vya klabu hiyo inayonolewa na kocha kutoka DR Congo Florent Ibenge.

Kisinda mwenye umri miaka 21 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo, ambayo pia imemsajili Clatous Chotta Chama kutoka kwa Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC.

Tayari Chama alishatambulishwa kuwa mchezaji halali wa klabu hiyo juma lililopita, na.ameshiriki katika mchezo wa kirafiki.

Kompany, Silva wajengewa sanamu jijini Manchester
Arteta awapigia magoti wachezaji Arsenal