Dunia haitomsahau Gabriel Villa, mwanasheria kwa taaluma aliyefanya pia kazi ya uwakala wa usafirishaji, ambapo Bwana huyu mwaka 1994 alikutana na mwanadada mrembo Christina Carta kwenye sherehe na wawili hawa wakapendana na hatimaye kufunga ndoa licha ya kuwa Gabriel alimzidi mrembo huyo miaka 30.

Tajiri huyo mara tu baada ya kufunga ndoa alimpeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominica kwenye visiwa vya nchi hiyo kula maisha kwa miezi minne na waliporudi waliishi pamoja kwenye ndoa ya furaha kubwa kwa miaka 20 na baada ya miaka hiyo ishirini ya kuishi pamoja hatimaye wawili hawa waligombana na Mwanamke akaenda kudai talaka kisheria, ili wagawane mali.

Gabriel Villa na Mkewe.

Lakini baada ya kufuatilia taratibu hizo za kisheria, Wanasheria wa Mwanamke huyo walimjulisha kuwa Gabriel alimtaliki mke wake huyo miaka 20 iliyopita bila yeye kujua hivyo kwa miaka yote hiyo hawakuwa wanaishi kwenye ndoa.

Kumbe ile fungate Gabriel aliyompeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominican alitumia pia mwanya huo kuandikisha talaka kabisa kwa mkewe bila mwenyewe kujua kwani kwa wakati huo ni nchi ya Jamhuri ya Dominican pekee ndiyo iliyokuwa inaruhusu kisheria talaka kutolewa bila mmoja wapo kujua.

Mwamba huyu alipoulizwa alisema alijua kuwa siku moja Mwanamke huyo angetumia mbinu ya kudai talaka, ili kuchukua mali zake hivyo alijiandaa mapema?

NDUGU YETU HUYU ANAPASWA KUPEWA CHEO GANI???

Dunia inakabiliwa na changamoto uaribifu wa maadili: Dkt. Mwinyi
Mkataba upanuzi Mkongo wa Taifa mawasiliano wasainiwa