Katika kuhakikisha inakuza ubunifu kwa kampuni changa za Teknolojia ya tabari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini, Tume ya Tehama (ICTC) imefanikisha safari ya wabunifu saba kwenda Algiers, Algeria kushiriki katika kongamano la kimataifa la Tehama barani Afrika litakaloshirikisha zaidi ya mataifa 50 kuanzia leo.

Kwa kushiriki katika kongamano hilo la siku tatu, wabunifu hao wa kitanzania watapata fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza kazi zao, kukutana na wataalamu wengine wa Tehama kutoka sehemu mbalimbali duniani ambako wanatarajiwa kujifunza kuelekea katika ukuaji wao kisekta.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Dkt. Nkuncwe Mwasaga, akizungumza jana jijini Dar es Salaam, alisema kwa Tume na taifa kwa ujumla, kongamano na maonesho hayo ni faida kubwa kwa. nchi kwani vitasaidia kukuza na kuvutia uwekezaji wa. Tehama
nchini.

“Hiyo ni hatua kubwa kwetu kama Tume ya Tehama lakini pia kwa nchi. Haya ni matunda ya uratibu wa programu ya kukuza kampuni changa za TEHAMA (ICT
Startups) ili kuwezesha bidhaa 2a TEHAMA kuingia katika soko na kuchangia katika kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa vijana. Tume imewezesha kampuni changakadhaa kuanza kutoa huduma,” alisema.

Kwa mujibu wa Pkt. Mwasaga, ushiriki katika kongamano hilo kubwa Afrika umewezeshwa na ICTC. Ameishukuru Serikali chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nguvu sekta ya tehama katika mpango wa kujenga uchumi wa kidigitali, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha safari ya wabunifu hao.

Katika kongamano hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na wabunifu 500, watazamaji zaidi ya 10,000, wa.wekezaji z00, wabobezi katika sekta ya tehama wapatao 100, kampuni za Tanzania zinazotarajiwa. kushiriki ni Ngasmake (Lipa kwa Ngasmake (Lipa kwa Uhakika),
Niajiri, Neuro-Sarufi AI, Simplitech, Mipango App, Scancode na Settlo.

Benki ya CRDB iliyoingia makubaliano na Tume ya Tehama kuendeleza Wabunifu wa Kampuni
ndogondogo za TEHAMA kupitia programu ya Imbeju, pia ni sehemu ya washiriki.

Naye Mkurugenzi wa Huduma 2a Ufundi wa Tume ya Tehama ambaye yuko Algeria na wabunifu hao, Jasson Ndanguzi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, akizungumzia manufaa ya ICTC kushiriki katika kongamano na maonesho hayo, alisema ni pamoja na
kusaidia kuvutia na kuongeza fursa 2a uwekezaji mitaji katika kampuni bunifu za TEHAMA nchini.

“Pia kuna fursa ya kuongeza ujuzi wa programu 2a uanzishwaji wa. vituo vya bunifu za TEHAMA nchini kwa kujifunza kutoka nchi zingine zinazoshiriki kongamano hilo, kupata washirika wa kuendesha programu 2a ubunifu wa kidijitali na kukuza soko la bidhaa za TEHAMA zinazotokana na bunifu za TEHAMA ili kukuza pato la taifa lakini pia kutangaza nafasi ya Tan2ania katika uwanda wa masuala ya bunifu za kidijitali.

“Na zaidi ya yote, ni fursa ya kuzitangaza kampuni changa zenye bunifu 2a TEHAMA ili ziweze kupata mitaji au/na washirika wa biashara nje ya mipaka ya Tanzania kama moja ya mkakati ya kukuza matumizi ya bunifu za TEHAMA nje ya nchi na hatimaye
kuongeza pato la fedha za kigeni,” alisema Ndanguzi.

Ukuzaji na kuvutia uwekezaji ni moja ya majukumu ya Tume ya Tehama inayotekeleza Sera ya Taifa ya Tehama pamoja na sera nyingine zinazohusiana na kuendeleza matumiziya tehama, lengo likiwa kutengeneza ajira na kuchangia katika shughuli za
kiuchumi na kijamii, huku ikiimarisha uratibu wa shughuli za Tehama ili kuongeza mchango wa sekta husika katika uchumi wa taifa.

Tume, kwa sasa inaelekeza nguvu katika kuanzisha vituo vya ubunifu wa Tehama kote
nchini, ikianza na mikoa ya Dar es Salaam,; , Arusha, Dodoma, Tanga, Mbeya, Lindi na Zanzibar, lengo likiwa kusogeza huduma karibu na wananchi, hasa
ikizingatiwa kumekuwa na ongez eko la uhitaji wa matumizi ya Teknolojia kwenye uchumi wa Tanzania.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 5, 2023
Joash Onyango avunja ukimya Singida FG