Tume ya Uchaguzi NEC na Viongozi wa vyama vya siasa wamekutana jijini Dar es Salaam ambapo lengo la kukutana ni kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku wakitumia mkutano huo kujadili namna ya kuboresha daftari la Kudumu la Wapiga Kura, pia mchakato wa uchaguzi mkuu ili kuhakikisha unakuwa huru na haki.
 
Akizungumza mbele ya viongozi wa vyama vya siasa, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa wadau na watanzania wanafahamu kuwa nchi ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
 
“Katika maandalizi hayo,Tume chini ya Ibara ya 74(6) ya Katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977 imepewa mamlaka ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya msingi ikiwa ni pamoja na jukumu la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara,” amesema Kaijage
 
Aidha, amesema kuwa NEC imeanza maandalizi ya mchakato wa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni mkakati wa kujiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2020.
 
Amefafanua kuwa kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 324 na ya kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa sura ya 292, Tume inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na uchaguzi mwingine unaofuata.
 
Pia ameongeza kuwa mchakato wa uhakiki wa vituo lililenga kuona kama kuna haja ya kuongeza vituo katika baadhi ya maeneo, vituo vilivyopo kama bado vinakidhi matakwa ya kisheria na kufanya marekebisho mengine kama kubadilisha majina ya vituo au kurekebisha majina ya vituo yaliyokosekana.
 
  • RC Dkt. Kebwe aagiza kukamatwa kwa waliovamia mashamba
  • JPM atoa neno kuhusu tukio la kutekwa kwa Mo Dewji
  • AAR yatoa matibabu bure kwa washiriki Kili Marathon 2019
 
Hata hivyo, Jaji Kaijage amesema kuwa matokeo ya uhakiki huo kwa Tanzania Bara yanaonyesha kuwa vituo vya kuandikisha wapiga kura vimeongezeka kutoka vituo 36,549 vilivyotumika kuandikisha wapiga kura mwaka 2015 hadi vituo 37,407.Vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka Kijiji/ Kata mmoja kwenda kata nyingine

Solari amkejeli Mourinho kuchukua nafasi yake, amlinganisha na mrembo
RC Dkt. Kebwe aagiza kukamatwa kwa waliovamia mashamba