Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia, Lazaro Samwel Nyalandu kujivua Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.

Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo, Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.

Wakati huo huo Waziri wa Tamisemi kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.

Hata hivyo, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.

Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo

Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi

NA. MKOA HALMASHAURI JIMBO
1. Singida Halmashauri ya Wilaya ya Singida Singida Kaskazini
2. Arusha Halmashauri ya Wilaya ya Longido Longido

Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi

NA. MKOA NA. HALMASHAURI NA. KATA
1. Kagera 1. Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. 1 Keza
2. Arusha 2 Halmashauri ya Jiji la Arusha 2 Kimandolu
3. Pwani 3.  Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 3 Kurui
4. Tabora 4. Halmashauri ya Wilaya ya Tabora
5 Kwaguni

4 Bukumbi
5. Tanga 5. Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
Video: Makonda atuma salamu kwa wanaume wa Dar
DC Kasesela awaweka mtegoni wasiotumia mashine za EFD