Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Elvis Mossy ametaka haki itendeke katika zoezi la upigaji na kuhesabu kura kwani wananchi wa jimbo hilo siyo watu wa vurugu.

Amesema kuwa kanuni zinahitaji watu wajae mita 100 baada ya kupiga kura lakini kama haki itatendeka wananchi wa Siha hawatakuwa na haja ya kulinda kura.

“Hatuna vurugu sisi. Kama wanataka turudi majumbani tutaenda tu. sisi tunachotaka ni haki, akishinda Mollel atangazwe lakini nikishinda mimi nitangazwe. Ila Kailima anajua kwamba kanuni zimeweka wazi mpiga kura anapaswa kukaa mita kadhaa baada ya kupiga kura,” amesema Elvis

Aidha, amesema kuwa mawasiliano yamekuwa kikwazo kikubwa kwani fomu za kura zimekuwa chache katika moja ya kituo lakini kila anapompigia Mkurugenzi hapokei simu ili kuweza kutatua changamoto hiyo.

Hata hivyo, taarifa zinasema katika jimbo la Siha watu mbalimbali wamejitokeza kupiga kura huku eneo la Sanya Juu wazee wakionekana kuwa wengi kuliko vijana.

 

Sanduku la kupigia kura laibiwa Kinondoni
Mgombea Ubunge Chadema akamatwa