Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amethibitisha kuwa chama hicho kimepokea barua y Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda yenye maelezo ya kujiondoa kwenye chama hicho baada ya muda wake wa ubunge kumalizika.

Akiongea na Jahazi ya Clouds Fm, Tundu Lissu amesema kuwa Shibuda aliwasilisha barua hiyo juzi lakini haikuwa na maana yoyote kwao kwa kuwa kujitoa kwenye chama ni hiari ya mtu yeyote na hakuna haja ya kuandika barua.

“Uanachama sio lazima, aliingia kwa hiari yake na ameondoka kwa hiari yake. Kwa hiyo sio suala la kuridhia kabisa. Hatuna uwezo wa kumwambia hapana hatutaki uondoke, hatuna uwezo huo,” alisema.

Aliongeza kuwa Shibuda anatafuta publicity kwa kuipeleka barua hiyo mwenyewe kwenye ofisi za chama hicho.
“Hiyo mbona ni hadithi ndogo sana. Ameandika na mjadala juu ya Shibuda sisi tumeshaumaliza miaka kadhaa ilyopita lakini kama ameandika tunaiweka tu kwenye faili tunaendelea,” alieleza Tundu Lissu.

Shibuda aliingia Chadema mwaka 2010 akitokea CCM. Chadema walimpa nafasi ya kugombea ubunge wa jimbo la Maswa Magharibi baada ya kuikosa nafasi hiyo kwa kushindwa katika kura za maoni za CCM.

Joto Dodoma: Mabaunsa Washawishiwa Kufanya Fujo Mgombea Asipopitishwa
Mzee Kingunge Aitahadharisha CCM, Atofautiana Na Nape