Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu amesema kuwa yupo tayari kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakao fanyika 2020.
Lissu ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na idhaa ya kiswahili ya BBC, ambapo amesema kuwa endapo chama chake pamoja na wananchi wakitaka agombee urais yupo tayari kufanya hivyo.
“Chama changu pamoja na vyama tunavyo shirikiana navyo, wanao tuunga mkono wakisema kuwa mimi nafaa kuwakilisha chama changu nipo tayari kufanya hivyo muda wowote,”amesema Lissu
Aidha, amesema kuwa vikao vya chama ndio vitakavyoamua nani atakayewakilisha chama hicho katika nafasi ya urais, hivyo hakuna mpambano wowote utakaojitokeza kwani hayo yatakuwa ni maamuzi ya mkutano mkuu ya kuchagua kama ni Lowassa, mwenyekiti Freeman Mbowe au yeye Tundu Lissu.
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA amesema kuwa wanaweza kuona Lowassa apumzike na kumpa nafasi kijana mwenye nguvu apambane kwani mapambano yaliyopo yanahitaji nguvu zaidi.
-
Polisi Njombe waeleza matukio ya utekaji na mauaji
-
Video: CAG amjibu Ndugai, anena mazito
-
Ndugai amlipua Zitto Kabwe, ‘Kiongozi muongo sana huyu’
Hata hivyo, ameongeza kuwa, atakubali kutokugombea Urais endapo vikao vya chama na wanachama wakisema bado hawezi kuwakilisha chama.