Mgombea wa kiti cha Urais wa Tanzania kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu amemaliza kutumikia adhabu yake ya kutokufanya kampeni kwa muda wa siku saba iliyotolewa na kamati ya maadili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa CHADEMA Taifa John Mnyika amesema kuwa Lissu ameanza kampeni zake leo Oktoba 10 Jijini Dodoma na kuelekea mkoa wa Singida.

Kwa upande wake Lissu akiwa wilayani Bahi mkoani Dodoma Lissu amesema iwapo chama hicho kitapewa idhini ya kuiongoza Tanzania kitarudisha uhuru wa wananchi kwani kunakosekana uhuru wa kuongea na kuhoji masuala ya maendeleo.

Amesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni muhimu na amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 ili kuamua hatima yao.

Lissu alisimamishwa kufanya kampeni na kamati ya kitaifa ya maadili ya uchaguzi baada ya kukiuka kanuni na Taratibu za Uchaguzi.

CHADEMA waitaka NEC kutaja kampuni inayochapisha karatasi za kura
Azerbaijan na Armenia zakubaliana kusitisha mapigano