Mwanasheria wa Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, Profesa George Wajackoya amethibtisha uwepo wa Lissu Nchini Kenye Jijini Nairobi kwaajili ya uzinduzi wa kitabu cha Vivuli- Bunge na uwajibikaji kwa Afrika Mashariki.

Akizungumza na mtandao wa Nation Africa leo Juni 24, 2021 Mwanasheria huyo amesema uzinduzi huo utafanyika katika hoteli ya Windsor nchini humo.

Katika kitabu chake, Lissu anaeleza historia ya mabunge ya Tanzania, Kenya na Uganda, akisimulia jinsi mabunge hayo yalivyotoka katika ukoloni wa Uingereza, pia anashauri mabunge hayo yawe na kivuli cha madaraka makubwa yaliyotolewa na watawala wa kikoloni na watawala waliokuja baada ya ukoloni.

Kitabu hicho kinakosoa mfumo wa utawala wa Rais na kimetumia fasihi kikibeba ujumbe kutoka kwenye historia ya kisiasa na Kikatiba ya nchi zote tatu.

Itakumbukwa Lissu ambaye liwahi kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi jijini Dodoma mwaka 2017, ambapo mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mara 25

Chuo Kikuu cha Mzumbe chafanya mahafali ndogo
ASFC: Historia ya Biashara Utd Vs Young Africans