Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka vijana na wahitimu wa Chuo Cha Sayansi Shirikishi Kilichopo Jijini Mbeya, kuepukana na vitendo vya utumiaji wa Dawa ya kulevya na mapenzi ya jinsia moja.
Malisa ameyasema hayo kwenye Mahafali ya tano ya Chuo hicho na kudai kuwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo vya mmomonyoko wa maadili, Vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vitendo hivyo.
Amesema, Wazazi na walezi wanatakiwa kutoona aibu Kuzungumza na watoto wao juu ya masuala ya Afya na Maadili, huku Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Cosmas Chacha akiishukuru Serikali kwa Kutoa kipaumbele kwenye sekta ya afya, kwa kukiwezesha chuo hiko kutoa elimu bora kwa wahitimu.
Kwa upande wake Mzazi, Criprian Haule amewataka wahitimu kutokata tamaa mara baada ya kuhitimu masomo yao na kuwataka kuwa na subira pale wanapokosa kazi na badala ya yake kujiajiri inapobidi ili kujikwamua kiuchumi.