Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi -CCM Jimbo la Mbeya Vijijini, kushirikiana na viongozi wa Serikali kulinda vyanzo vya maji.

Malisa ameyasema hayo kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Jimbo la mbeya Vijijini, uliofanyika hivi kaaribuni katika ukumbi wa Lehner uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Amesema, Mkoa wa mbeya una milima mingi ambayo ni kikwazo cha upatikanaji wa maji na hata kama yakipatikana chini ni gharama kubwa kuyafikisha kwa wananchi, hivyo vyanzo vichache vilivyopo viwekewe mkakati wa makusudi wa kuvilinda.

Sehemu ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.

Hata hivyo DC Malisa amesema viongozi wa chama ndio wanaoishi na wananchi kwa ukaribu na ndio wanaojua kwa ukaribu zaidi watu wanaoharibu vyanzo hivyo vya maji na kwamba wanauwezo wakutoa taarifa pindi wanapoona kuna uharibifu.

Aidha, Malisa pia amesema Serikali ya Rais Samia imetoa kipaumbele kikubwa katika sekta ya maji, hivyo viongozi wana kila sababu ya kulinda vyanzo na miundombinu hiyo, ili yawafikie wananchi kwa uhakika.

Che Fondoh Malone kimeeleweka Simba SC
CCM, RPF - Inkotanyi wakutana Lumumba