Rais wa mpito wa FC Barcelona Carlos Tusquets amesema kulikua na umuhimu wa kumuuza nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Lionel Messi, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Tusquets, ametoa kauli hiyo alipohojiwa na kituo cha Redio cha RAC1, ambapo alisema kama angekua Rais kwa wakati huo, asingesita kumuuza Messi ambaye alikua anahusishwa na mpango wa kusajiliwa Manchester City.

Kiongozi huyo amesema kutokana ya kiuchumia ambayo FC Barcelona wanaipitia kwa sasa, anaamini kuuzwa kwa mshambuliaji huyo kungefanikisha mambo mengi kwenda vizuri klabuni hapo, hasa mishahara ya wachezaji na watendaji wengine.

“Hii ingekua sehemu kubwa ya mishahara na ingeongeza mapato kwa kiasi kikubwa. Lakini hili ni suala ambalo makocha wanatakiwa kuliridhia, hiyo sio sehemu yangu.”

 “Kwa sasa, LaLiga ndio wanaopanga viwango vya mishahara, ila kwa sababu hiyo ingesaidia.”

Mapema mwezi Agosti, Lionel Messi aliomba kuondoka FC Barcelona kwa sababu kadhaa, lakini mpango huo ulikwama kufautia uongozi wa klabu hiyo kwa wakati huo kuweka ngumu, huku ukisaidiwa na Shirikisho als oka nchini Hispania.

Dar yapiga hatua matumizi njia za uzazi wa mpango
New Habari 2006 yasitisha uzalishaji wa magazeti yake