Mgombea wa uraisi kwa tiket ya chama cha Mapinduzi (CCM) Dokta. John Magufuli ameahidi kukamilisha uimarishaji wa mifumo ya kisera na kisheria ili kuwezesha wanachi na taifa kwa ujumla kunufaika na utajiri wa madini .

Akiwawahutubia  wananchi wa mkoa wa shinyanga ameseama kuwa chama chake cha CCM kitaka wananchi wa kawaida wachimbe madini wenyewe na kunufaika na Madini na rasilimali zote .

“Kwa mchango wa sekta ya madini tutaongeza pato la taifa kutoka aslimia 3.4 hadi ifikie asilimia 5.1 kwa mwaka,” alisema Magufuli

Magufuli amesema kuwa serikali yake itaimarisha mazingira usimamizi wa  mifumo ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo kupata leseni pamoja na mikopo ya kuendeshea shughuli za uchimbaji .

Griezmann ahakikishiwa nafasi FC Barcelona
JPM awatumia ujumbe waliokatwa CCM

Comments

comments