Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting,  Masau Bwire amesema kuwa kikosi chake kiko imara licha ya kufungwa goli saba na wekundu wa msimbazi lakini kwake si tatizo, bali kikosi hicho kitafanya maajabu makubwa katika msimu huu.

Amesema kuwa kufuatia kipigo hicho cha goli saba kutoka kwa Klabu ya Simba, hawajakata tamaa kwani bado kuna nafasi ya kufanya vizuri katika mechi  mbalimbali za ligi Kuu Tanzania Bara  2017/2018.

‘Tutawashangaza watu kuwa ni sisi kweli tulifungwa saba, mwalimu ameona makosa anayafanyia kazi na hata wachezaji wameona kilichotokea wanajua wanapaswa kufanya nini”,amesema Masau Bwire

Aidha, Kabla ya mechi dhidi ya Simba, Masau Bwire ambaye ni mwalimu kitaaluma alijigamba sana wangeiangusha Simba, lakini mambo yakaenda tofauti na kupigwa goli saba na Simba

Hata hivyo, Mashabiki wengi wa Simba walikuwa na wasiwasi kutokana na maneno ya Masau Bwire lakini baada ya ushindi huo mnono nao pia wamejipa imani ya kufanya vizuri zaidi katika michezo iliyopo mbele yao.

FIFA yawarudisha uwanjani Senegal na Afrika Kusini
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 8, 2017