Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wananchi waungane na Serikali pamoja na Wadau mbalimbali wa maendeleo, katika kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu na kuzuia maambukizi mapya pamoja na vifo visivyo vya lazima.

Majaliwa ameyasema hayo hii leo Machi 24, 2023 wakati akizungumza na Wannchi katika siku ya maadhimisho ya kifua kikuu Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa bariadi,  Mkoani Simiyu.

Amesema, “kila mmoja wetu anao wajibu wa kuhakikisha anachukua hatua zote za tahadhari kwani Mgonjwa mmoja wa kifua kikuu ambaye hajagunduliwa na hakuwekwa kwenye utaratibu wa matibabu ana uwezo wa kuambukiza Watu kati ya 10 mpaka 20 kwa mwaka.”

” Nitoe rai kwa kila Mwananchi kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya na Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa katika kujilinda dhidi ya ugonjwa huu,” ameongeza Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu pia amesema kutokana na hatua zinazochukuliwa na Serikali, Tanzania imepiga hatua katika kutokomeza kifua kikuu nchini.

Majaliwa ameongeza kuwa, “takwimu za shirika la Afya Duniani zinaonyesha kuwa kwa Mwaka 2022,  vifo vinavyosababishwa na kifua kikuu vimepungua kutoka 55, 000 mwaka 2015 hadi 25, 800 sawa na asilimia 55.”

“tumepunguza maambukizi mapya ya kifua kikuu kutoka wagonjwa 306 katika kila hidadi ya Watu 100, 000 na kufikia Wagonjwa 208 katika kila Watu 100, 000 ikiwa ni sawa na kupungua kwa asilimia 32,” amefafanua Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Majaliwa pia amewaaagiza  Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia kwa karibu fedha za ununuzi wa dawa zinazotolewa kila mwezi, ambazo ni wastani wa Shilingi 17 Bilioni na katika kipindi cha miaka miwili, Bilioni 462 zimetumika.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 25, 2023
Meridianbet yaunga mkono juhudi za Jeshi la Polisi