Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba endapo angepata nafasi ya kuongoza sekta ya elimu angeshauri kufumua mitaala na kuweka somo la kumfundisha mtoto namna ya kuitafuta hela badala ya kumzoesha kuomba hela ili aweze kumudu maisha ya baadaye.

Kishimba ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Dar24 Media na kuongeza kuwa hakuna ubaya kumfundisha mtoto namna ya kutafuta kitu na namna pesa inavyotafutwa kwani itamsaidia kujua matumizi na kuhifadhi akiba ili aweze kumudu hali ya uchumi na kujiendeleza kimaisha.

Amesema, ni muhimu kuweka bidii ya kuwafundisha watoto umuhimu na uhalisia wa maisha yaliyopo mtaani, kwani wengi wao wamekuwa wakikosa ajira na hivyo kujikuta na wakati mgumu wa kile walichojifunza shuleni kukitumia uraiani.

“Maana yake hata ukikataa kumfundisha asbuhi atakuomba hela ya Soda, je ukimfundisha yeye kutafuta hela ya soda kutakuwa na ubaya gani, je akijua hela madhara yake huwa nini, atakuwa tu mfanyabiashara na atatunza hela ndiyo ‘logic’ yake,” amesema Kishimba.

Aidha, Kishimba ambaye amekuwa akipigania uboreshaji wa mfumo wa Elimu nchini ameongeza kuwa haileti maana kumfundisha mtoto kuomba hela na badala yake aelekezwe jinsi ya kuipata kwaniitamsaidia katika kujikomboa na hali ngumu inayowakabili mara baada ya kumaliza elimu.

Mpaka pori la akiba: Wananchi watakiwa kufuata utaratibu
Fahamu madhara ya pambo la Dhahabu kwa Mwanaume