Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ imetangaza rasmi tarehe ya Sherehe ya utoaji Tuzo kwa msimu wa 2021/22, baada ya kumalizika kwa michezo ya Ligi Kuu juzi Jumatano (Juni 29) katika viwanja vinane tofauti.
TPLB imetaja Julai 07 kuwa siku maalum ya Shehere hizo, zitakazofanyika katika Hoteli ya Rotana jijini Dar es salaam, huku ikitoa orodha ya wachezaji, makocha, waamuzi na timu ambazo zinawania tuzo mbalimbali.
Kwa mara ya Kwanza katika sherehe hizo kutakua na Tuzo Mchezaji Bora wa Ligi Daraja la Kwanza (Championship) sambamba na Tuzo ya mhezaji Bora wa Ligi Daraja la Pili (First League).
Miaka ya nyuma wachezaji waliokuwa wanatajwa kama wachezaji Bora walikua wakipewa Tuzo zao baada ya Michuano ya ligi zao kufikia tamati, lakini kwa mwaka huu, watajumuika na wenzao wa Ligi Kuu na Ligi Kuu ya Wanawake katika ukumbi mmoja.
Mchanganuo wa Tuzo za TFF ni kama ifuatavyo
- Mshindi wa Pili wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ – Coastal Union, Young Africans
- Bingwa wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ – Coastal Union, Young Africans
- Mshindi wa tatu Ligi Kuu ya Wanawake – Yanga Princess
- Mshindi wa Pili Ligi Kuu ya Wanawake – Fountain Gate Princess
- Mshindi wa Kwanza Ligi Kuu ya Wanawake – Simba Queens
- Mshindi wa Nne Ligi Kuu ya Wanaume – Geita Gold FC
- Mshindi wa Tatu Ligi Kuu ya Wwanaume – Azam FC
- Mshindi wa Pili Ligi kuu ya Wanaume – Simba SC
- Bingwa Ligi Kuu ya Wanaume – Young Africans
- Mfungaji Bora Kombe la Shirikisho – Abdul Seleman (Coastal Union-Mabao 6), Heritier Makambo (Young Africans-Mabao 3)
- Mfungaji Bora Ligi Kuu Wanawake – Asha Djafar (Mabao 27)
- Mfungaji Bora Ligi Kuu Wanaume – George Mpole (Mabao 17)
- Timu yenye Nidhamu Ligi Kuu Wanawake – Yanga Princess, JKT Queens na Alliance Girls
- Timu yenye Nidhamu Ligi Kuu Wanaume – Tanzania Prisons, Young Africans, Simba SC
- Meneja Bora wa Uwanja – Sikutu Kilakala (Azam Complex), Mwaluka Modestus (Uwanja wa Sokoine) na Godfrey Kombe (Manungu Complex)
- Kamisha Bora Ligi Kuu Wanawake- Abousufian Silia (Iringa) Aboubakar Kazinja (Kagera) na Somoe Ng’itu (Dar es salaam)
- Seti Bora ya Waamuzi Ligi Kuu Wanaume – MN 160 (Young Africans Vs Simba SC), MN 64 (Simba SC Vs Young Africans) na MN 120 (Mtibwa Sugar VsYoung Africans)
- Mwamuzi Msaidizi Bora Ligi Kuu Wanawake – Zawadi Yusuph (Dar es salaam), Sikudhan Mkulungwa (Njombe) na Glory Tesha (Dar es salaam).
- Mwamuzi Msaidizi Bora Ligi Kuu Wanaume – Frank Kombe (Dar es salaam), Mohamed Mkono (Tanga) na Janeth Balama (Iringa)
- Kocha Bora Ligi Kuu Wanawake – Sebastian Nkoma (Simba Queens), Masoud Juma (Fountain Gate Princess) na Edna Lema (Yanga Princess)
- Kocha Mkuu Bora Ligi Kuu Wanaume – Nasreddine Nabi (Young Africans), Fred Minziro (Geita Gold) na Juma Mgunda (Coastal Union)
- Tuzo ya Chipukizi Bora Ligi Kuu Wanawake – Clara Luvanga (Yanga Princess), Frida Gerald (Fountain Gate Princess) na Winfrida Charles (Alliance Girls)
- Tuzo ya Chipukizi Bora Ligi Kuu Wanaume – Dickson Mhilu (Kagera Sugar), Tepsie Evance (Azam FC) na Richardson Ng’odya (Mbeya City)
- Tuzo ya Fair Play Ligi Kuu Wanaume – Itatangazwa Ukumbini
- Mwamuzi Bora Ligi Kuu Wanawake – Tatu Malongo (Tanga), Amina Kyando (Morogoro) na Esther Adabert (Tanga)
- Mwamuzi Bora Ligi Kuu Wanaume – Ramadhan Kayoko (Dar es salaam), Ahmed Arajiga (Manyara) na Elly Sasii (Dar es salaam)
- Golikipa Bora ASFC – Mohamed Mohamed (Coastal Union), Djigui Diara (Young Africans) na Beno Kakolanya (Simba SC)