Tuzo za Grammy 2022 zimerejea tena baada ya kusitishwa kwa muda kwa sababu za kiafya ikiwa ni wakati wa maambukizi ya juu ya kirusi Omicron na kuepuka kuenea kwa Covid-19.
CBS na Recording Academy wametangaza kuwa tukio la utolewaji wa tuzo hizo litafanyika huko Las Vegas nchini Marekani siku ya jumapili April 3.
Tuzo za Grammy hapo awali ilikuwa zifanyike Crypto.com Arena iliyopo Los Angeles Januari 31, lakini iliahirishwa kutokana na sababu zilizotajwa kuwa ni kuepuka hatari ya maambuki ya virusi vya Covid-19 kutokana na kuripotiwa kwa visa vipya kadhaa nchini humo.
Mkurugenzi mtendaji wa Recording Acardemy Harvey Mason Jr. Akiongea na CNN alisema “Tunafuraha kuipeleka hafla ya tuzo za Grammy Las Vegas kwa mara ya kwanza, na kuifanya kwa ukubwa wa viwango vya dunia.”
“Tangu tumetangaza kuahirisha tarehe maalumu ya hafla, tumekuwa tukipokea jumbe za kutuunga mkono kutoka kwenye jamii za wasanii, tumenyeyekezwa na ukarimu wao, tunashukuru kwa kujitolea bila kuyumbayumba” aliongeza.
Trevor Noah, mchekeshaji na host “The Daily Show” ametangazwa kama mshereheshaji mkuu wa hafla hiyo kwa mara nyingine tena.