Bondia kutoka Morogoro, Twaha Kiduku amemaliza ubishi kwa kumpiga Dullah Mbabe katika pambano la raundi kumi lililoshuhudiwa usiku wa kuamkia leo, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kiduku alionekana kuwa mbele kwa alama kwa mujibu wamatokeo rasmi yaliyotangazwa, huku pambano hilo likivuta umakini wa watazamaji wakati wote.

Majaji walitoa alama 193-97, 91,99 na 93-97, wote wakimpa ushindi Twaha Kiduku.

Pambano hilo lililokuwa na ushandani mkubwa, lilianza kwa kasi huku wengi wakiamini halitafika raundi 10. Hata hivyo, uwezo wa mabondia hao wa kumudu ‘vitasa’ vya moto ulibadili utabiri huo.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Kiduku alisisitiza kuwa maandalizi yake ndio siri ya mafanikio.

“Asante sana namshukuru Mwenyezi Mungu. Na kikubwa ilikuwa kumuomba Mungu na bidii,” alisema Kiduku.

Mabondia Hassan Mwakinyo na Mfaume Mfaume walipamba tukio hilo kama wachambuzi kupitia kituo cha runinga cha Azam.

Muigizaji wa ‘Black Panther’, Boseman afariki dunia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 29, 2020

Comments

comments