Endapo Bondia wa Tanzania Twaha ‘Kiduku’ Kassim atafanikiwa kumchapa Iago Kiziria kutoka Georgia keshokutwa Jumamosi (April 22) atakuwa bingwa wa mikanda miwili kwa mpigo.
Pambano hilo la uzani wa juu mwepesi, litaunguruma mjini Morogoro, huku watanzania wengi wakiamini Twaha Kiduku ana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea kutokana na rekodi ya michezo yake ya hivi karibuni…
Kiduku bondia namba moja nchini kwenye uzani wa super middle, atacheza nyumbani kwenye Ukumbi wa Tanzanite, Morogoro, kuwania mataji ya UBO International na PST katika pambano la raundi 10 la uzani wa super middle.
Kiziria, ambaye hajawahi kupigwa kwa Knock Out (KO) wala Technical Knock Out (TKO) aliwasili jijini Dar es Salaam jana na kisha kwenda Morogoro tayari kwa zoezi la kupima uzito litakalofanyika kesho Ijumaa (April 21).
Promota wa pambano, Selemani Semunyu amesema Mtanzania mwingine, Loren Japhet anayeishi Ghana pia aliwasilia jana na leo ataelekea Morogoro. Loren atazichapa na Juma Choki, kuwasindikiza Kiduku na Kiziria.
Kocha wa bondia huyo, Pawa Ilanda alisisitiza kufanya mazoezi ya kutosha kucheza raundi zote 10.