Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi tarehe 24 Oktoba, mwaka huu nchini Malawi.

Mechi hiyo kati ya Twiga Stars dhidi ya Malawi itachezwa jijini Lilongwe kufuatia mwaliko wa chama cha soka nchini Malawi (FAM) kuialika Twiga Stars kwenda nchini Malawi kwa ajili ya mchezo huo

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya vikosi vya timu zote mbili za Wanawake Tanzania na Malawi kwa ajili ya michuano mbalimbali.

Lowassa Aeleza Kama Atakubali Matokeo Akitangazwa Ameshindwa!
Karuma Kuhudhuria Kongamano La FIFA