Timu ya taifa ya soka ya wanawake, ‘Twiga Stars’ leo Jumanne (Oktoba 31) inashuka dimbani ugenini Gaborone kucheza na Botswana kwenye mchezo wa marudiano wa Olimnpiki (WOFT) 2024 Paris, Ufaransa.
Twiga Stars inahitaji sare au ushindi kufuzu hatua ya nne kwani mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi walishinda 2-0.
Endapo Twiga Stars watafuzu hatua ya tatu wataungana na Zambia ‘She-Polopolo’, wawakilishi wa Afrika katika fainali zilizofanyika Jiji la Tokyo nchini Japan, ambao walifuzu raundi ya tatu kutokana na kuondolewa kwa Mali na timu nyingine sita kufanya idadi ya timu nane.
Akizungumzia mchezo huo Kocha Mkuu wa timu za taifa za wanawake, Bakari Shime amesema watacheza kwa kushambulia na kuzuia pia kwa sababu wanahitaji ushindi mara mbili ya wapinzani wao.
“Tutaingia kwenye mchezo kwa kushambulia na kuzuia pia kwa sababu tunahitaji ushindi ili kusonga mbele,” amesema Shime.
Amesema makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ameyafanyia kazi baada ya kuona wapinzani wao wanavyocheza.
Baada ya kucheza Raundi ya tatu, zitapatikana timu nne ambazo zitamemyana katika raundi ya nne, Washindi wawilli wa raundi ya nne watafuzu kucheza Michuano ya Olimpiki jijini Paris-Ufaransa mwakani.