Timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake (Twiga Stars) imeendelea na maandalizi ya mashindano ya CECAFA kwa Wanawake  yatakayofanyika nchini humo kuanzia Novemba 16-28 mwaka huu.

Michuano hiyo inayoshirikisha Nchi za afrika mashariki na kati,inaandaliwa na Baraza la vyama vya soka la nchi za Afrika mashariki na kati (CECAFA).

Tanzania itaanza michuano hiyo kwa mara ya kwanza huku timu yake ya taifa Twiga Stars ikiwa bingwa mara mbili mfululizo, ambapo kwa mara ya kwanza michuano hiyo ilifanyika nchini Uganda na mwaka uliofuata Rwanda walikua wenyeji.

Safari ya mafanikio ya Twiga Stars Ilianza chini ya kocha sebastian nkoma, pale walipolichukuwa taji la michuano hiyo mwaka 2016 nchini Uganda,na sasa Timu hiyo ipo chini ya Kocha Bakari shime,na wachezaji wa Timu hiyo wametamba Kulichukuwa kwa mara ya Tatu Kombe hilo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 23, 2019
Makonda atengua kauli ya Mjema, ''Marufuku kufanya ibada katikati ya wiki''