Baada ya ‘drama’ ya wiki kadhaa iliyozua gumzo mitandaoni, Tyrese amewaomba radhi mashabiki wake.

Muigizaji huyo Fast & Farious ameibuka wikendi iliyopita akionesha kujutia kuweka video zinazomuonesha akilia kama mtoto akilalama kuwa mkewe amemzuia kumuona mwanae.

Tyrese ametupia lawama dawa za kupambana na msongo wa mawazo alizopewa na daktari bingwa wa magonjwa ya akili.

“Nilikuwa na msongo wa mawazo kuhusu kumkosa binti yangu? Ndiyo. Lakini nilimuona mmoja kati ya wataalam wa magonjwa ya akili ili nipate msaada, alipendekeza nitumie dawa fulani, na dawa hizo ndizo zilizonivuruga,” alisema Tyrese.

 

Alisema kama watu wanamfahamu vizuri wanafahamu kuwa kuna kitu hakikuwa sawa na kwamba hakuwa katika hali ya kawaida kiakili.

Msanii wa Bongo Movie Lulu Michael ahukumiwa kwenda jela
Davido anyakua tuzo ya 'MTV EMA'